Njia mbalimbali hutumika katika kukusanya madeni toka kwa Wateja (Tukizingatia kwamba, huduma ya maji hutolewa kwa mkopo na Wateja hulipa baada ya kupelekewa madai/ankara zao), njia hizi ni kama ifuatavyo;
- Kuwataarifu Wateja umuhimu wa kulipa Ankara zao mapema kupitia redio, matangazo ya spika za magari na kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi.
- Kuwatumia Wateja notisi za kusitisha huduma, hii hutumika zaidi kwa Taasisi.
- Kuwapa Wateja wenye madeni makubwa muda wa kulipa madeni yao usiozidi miezi mitatu.
- Na hatua ya mwisho ni SHUWASA kusitisha huduma kwa Mteja.
Njia hizi huzingatia Sera ya madeni ya Mamlaka.