Inachakata...
Alhamisi, Hufungua 01:30 - 10:30 (Isipokuwa sikukuu za umma)

Vyanzo vya Maji


Vyanzo vya Maji na Uwezo Wake

Mamlaka ina vyanzo vya aina tatu vya maji ambavyo ni; Bwawa la Ning'hwa, visima vya maji Tinde na Bushora, pamoja na maji kutoka ziwa Viktoria. Maji kutoka ziwa Viktoria ndiyo chanzo kikuu cha maji kwa Mamlaka.


Bwawa la Ning’hwa

Kabla ya kutekelezwa mradi wa maji kutoka ziwa Viktoria, Bwawa lilikuwa chanzo kikuu cha maji tkatika Manispaa ya Shinyanga likiwa na uwezo wa mita za ujazo 10,600,000 na kuzalisha mita za ujazo 10,000 kwa siku. Kina cha Bwana kinategemea sana na kiwango cha mvua kwa mwaka.


Maji ya Jumla

Mamlaka inanunua maji yaliyotibiwa kutoka ziwa Viktoria ambayo yanasambazwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA). Hiki ndiyo chanzo kikuu cha maji kwa sasa.


Na. Chanzo Ujazo (m3 kwa Siku)
Undaji Sasa
1. Bwawa la Ning’hwa 8,000 7,500
2. Maji ya Ziwa Viktoria 80,000 40,000
3. Visima vya Maji 100 40
Jumla: