Mpaka mwishoni mwa mwezi Aprili 2023, SHUWASA ilikuwa na jumla ya Wateja 28,585.
Mamlaka inatekeleza mikakati iliyojiwekea katika kuhakikisha kwamba, huduma kwa Wateja inaendelea kuwa bora na kufikia viwango vilivyowekwa na mthibiti/Msimamizi wa Sekta (EWURA) Sehemu kubwa ya Wateja wa SHUWASA ni Wateja wa Majumbani ambao wanatumia maji kwa 70.7% ya maji yanayozalishwa na Mamlaka na sehemu inayobaki 29.3% ni kiwango cha maji kinachotumiwa na Wateja wa makundi mengine Kwa upande wa mapato, kundi la Wateja wa Majumbani linaiingizia Mamlaka mapato kwa 64.4%.