Inachakata...
Jumapili, Imefungwa

Haki na Wajibu


Haki

Wateja wetu wana haki zifuatazo:-

  • Kupatiwa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa mujibu wa sheria.
  • Kupatiwa taarifa sahihi na kwa wakati.
  • Faragha na siri kwenye nyaraka na huduma aliyopewa.
  • Fursa ya kupata taarifa zinazohusu utendaji wa Mamlaka.
  • Kutoa maoni juu ya ubora huduma zetu.
  • Kutumia /kutoa /kuwasilisha malalamiko kwenye ngazi ya juu endapo hakuridhika na uamuzi uliotolewa kwa malalamiko yake.
  • Haki ya kurekebisha taarifa


Wajibu

Wateja wetu wanaweza kutusaidia kuwapa huduma bora kwa kufanya yafuatayo:-

  • Kuwawapa wafanyakazi wetu heshili stahili.
  • Kutoa taarifa kamili, sahihi na kwa wakati kuhusiana na huduma za Mamlaka kama zinavyohitajika.
  • Kuzingatia mahitaji ya kisheria wakati wa kuomba na kutumia huduma.
  • Kulipa ankara za huduma kwa wakati.
  • Kushirikiana na Wafanyakazi.
  • Kuzingatia amri na maagizo ya Mamlaka.
  • Kutokutoa rushwa au zawadi kwa lengo la kupata upendeleo.
  • Kutoa maoni juu ya Huduma za Mamlaka.