Maadili
Tunaamini kuwa Dhima na Dira yetu itafanya kazi vizuri kwa kutambua na kusimamia maadili yetu kikamilifu.
Wajibu Wetu- Kwa Wateja
- Kutoa huduma bora ya majisafi na usafi wa mazingira kwa kukidhi mahitaji
- Kuendelea kuwekeza na kuibua huduma bora za maji zenye thamani ya fedha
- Kufikia mahitaji ya wateja kwa wakati na kikamilifu.
- Kuanzisha mahusiano endelevu na ya muda mrefu na wateja wetu.
- Kwa Wafanyakazi
- Kuvutia na kudumu na wafanyakazi
- Kuheshimu wafanyakazi na haki zao
- Kutoa kazi katika mazingira ya wazi na ya kushirikiana.
- Kuhimiza ubunifu na uvumbuzi katika kila nyanja ya kazi.
- Kutoa fursa ya ukuaji kwa wafanyakazi wote ndani ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Maji ya Shinyanga.
- Kuhimiza wafanyakazi kufanya mapendekezo ya kuboresha ufanisi wao na wa Mamlaka.
- Kutoa mazingira mazuri kazi kwa kuzingatia afya, usalama na yenye kufurahisha.
- Kwa Wazabuni
- Kufanya kazi na wazabuni kwa usawa
- Kutambua na kuzingatia maslahi kwa pamoja
- Kuwawezesha wazabuni kuendeleza biashara zao wakati wowote iwezekanavyo.
- Kuanzisha uhusiano endelevu na wa muda mrefu na wazabuni wetu.
- Kwa Shinyanga
- Kutoa ajira kwa jamii
- Kuwa kama chanzo cha maji kwa maisha ya kila siku
- Kuhimiza na kuendeleza vipaji vya asili
- Kusaidia jamii kupitia matukio maalum n.k