Water Sources
Mamlaka ina vyanzo vya aina tatu vya maji ambavyo ni; Bwawa, visima na maji kutoka ziwa viktoria. Maji kutoka ziwa viktoria ndiyo chanzo kikuu cha maji kwa Mamlaka.
- Bwawa la Ning'hwa
- Kabla ya kutekelezwa mradi wa maji kutoka ziwa Viktoria, Bwawa lilikuwa chanzo kikuu cha maji tkatika Manispaa ya Shinyanga likiwa na uwezo wa mita za ujazo 10,600,000 na kuzalisha mita za ujazo 10,000 kwa siku. Kina cha Bwana kinategemea sana na kiwango cha mvua kwa mwaka.
- Maji ya Jumla
- Mamlaka inanunua maji yaliyotibiwa kutoka ziwa Viktoria ambayo yanasambazwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA). Hiki ndiyo chanzo kikuu cha maji kwa sasa.
Na. | Chanzo | Uwezo M3 kwa Siku | |
---|---|---|---|
Undaji | Sasa | ||
1 | Bwawa la Ning’hwa | 8,000 | 7,500 |
2 | Maji kutoka Ziwa Viktoria | 80,000 | 40,000 |
Jumla | 88,000 | 47,500 |