Mfumo wa Majitaka
Kwa sasa mamlaka haina mfumo wa uondoaji majitaka na kupelekea huduma ya uondoaji majitaka kufanywa na Manispaa ya Shinyanga kupitia idara ya afya.
Katika mpango wa maendeleo wa sekta ya maji (WSDP) awamu ya kwanza mtalaam muelekezi ambaye ni GIBB Afrika amekamilisha kazi ya kuandaa makablasha ya miundombinu hiyo na kuwasilisha wizara ya maji kwa hatua zaidi.
Matarajio yaliyopo ni kwamba, katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa sekta ya maji awamu ya pili (WSDP II) na kama fedha itapatikana ujenzi wa mfumo wa uondoaji majitaka unaweza kutekelezwa.