Haki na Wajibu
Wateja wetu wana haki zifuatazo:-
- Kupatiwa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa mujibu wa sheria
- Kupatiwa taarifa sahihi na kwa wakati
- Faragha na siri kwenye nyaraka na huduma aliyopewa
- Fursa ya kupata taarifa zinazohusu utendaji wa Mamlaka.
- Kutoa maoni juu ya ubora huduma zetu
- Kutumia /kutoa /kuwasilisha malalamiko kwenye ngazi ya juu endapo hakuridhika na uamuzi uliotolewa kwa malalamiko yake.
- Haki ya kurekebisha taarifa
Wateja wetu wanaweza kutusaidia kuwapa huduma bora kwa kufanya yafuatayo:-
- Kuwawapa wafanyakazi wetu heshili stahili
- Kutoa taarifa kamili, sahihi na kwa wakati kuhusiana na huduma za Mamlaka kama zinavyohitajika
- Kuzingatia mahitaji ya kisheria wakati wa kuomba na kutumia huduma
- Kulipa ankara za huduma kwa wakati
- Kushirikiana na Wafanyakazi
- Kuzingatia amri na maagizo ya Mamlaka
- Kutokutoa rushwa au zawadi kwa lengo la kupata upendeleo
- Kutoa maoni juu ya Huduma za Mamlaka