Usambazaji Maji
Mamlaka imegawanya eneo lake la huduma katika kanda nne; Kanda ya Kati, Kanda ya Kaskazini, kanda ya Kusini na Kanda ya Mashariki. Matandao wa mabomba una urefu wa km 548.24 yanayounganisha kanda zote nne. Mfumo mpya (Maji kutoka ziwa viktoria) una urefu wa km338.74 wenye mabomba ya uPVC na chuma ya kuanzia kipenyo cha mm110, Maji hupelekwa kwenye matanki manne yaliyo kwenye miinuko ndani ya Manispaa ya Shinyanga kwa urefu wa km27 yenye vipenyo kati ya mm400 hadi mm900. Matanki yamewekwa kwenye miiniuko kwa lengo la kupata mgandamizo wa maji unaotakiwa kusambaza maji katika Manispaa yote. Matanki haya yana mitaza ujazo 250 kila moja yenye uwezo wa kusambaza maji kama ifuatavyo:-
Na. | Kanda | Urefu wa mtandao (km) |
---|---|---|
1 | Kanda ya Kati | 140.47 |
2 | Kanda ya kusini | 137.48 |
3 | Kanda ya Kasikazini | 68.94 |
4 | Kanda ya Mashariki | 16.90 |
5 | Mfumo wa zamani | 184.45 |
Jumla | 548.24 |